Loading...
 

Historia Yetu

 

Agora ilianzishwa rasmi Agosti 21, 2016,  kwa tangazo la Facebook kutoka kwa Alexander Hristov. Kila mwaka, tunasherekea siku ya kuanzishwa Agora kwenye Agora International Convention.

Japokuwa tangazo la mwanzo lilizungumzia "muundo wa ada wa kimo cha chini" (ambao mwanzoni ulikuwa unategemea na kiwango cha "per-capita GDP" (wastani wa pato la taifa kwa kila mwananchi) cha kila nchi), ada zilitolewa mwaka 2016 na 2017. Mwishowe, mwaka 2018, ilitangazwa kuwa, kiukweli, Agora itakuwa bure kwa klabu zote za umma. Muundo wa kiuchumi ulibadilika kuwa mmoja ambao unategemea michango, ruzuku za serikali, malipo kutoka klabu za shirika, na kozi za kitaaluma. Daima Agora imekuwa na dira kubwa sana ya mabadiliko kabambe - zaidi ya uzungumzaji wa mbele ya hadhira - na faida za kuweza kufikia watu wengi, kila mahali, bila kujali kiwango chao cha kipato au daraja lao la kijamii, na kuwasaidia kuwa viongozi wa baadae kwa kiwango kikubwa sana kilishinda upotevu wa mapato.

Mwanzo wetu haukuwa mwepesi - nyenzo zote za kielimu zilibidi ziandikwe kutoka mwanzoni. Mfumo mpya wa kielimu ilibidi utengenezwe, miundombinu mipya kabisa ya teknolojia ya habari (IT), seti mpya kabisa ya chaneli za mitandao ya kijamii.

Kwa kuongozea kwenye "maumivu ya kuanzilishwa" yaliyotarajiwa, tulipitia baadhi ya ugumu usiotarajiwa - mashirika shindani waliiona Agora kama kitisho kwenye muundo wa wa kibiashara: tulikuwa tunatoa bure kitu ambacho walikuwa wanatoza, kwa miongo mingi, na wanachama wa mashirika hayo waligundua na wakawa wanahamia Agora.

Mwanzilishi na wafuasi wengi wa mwanzoni walitukanwa, walitumiwa barua za chuki, vitisho binafsi, na hata vitisho rasmi vya kisheria kutoka mawakili wa ngazi ya juu wa ndani ya nchi vya kuacha. Watu wenye nafasi za uongozi ndani ya mashirika mengine waliombwa waachie nafasi zao kwa kuonyesha msaada kwa Agora. Tulipitia pia uharibifu na hujuma za ndani ya shirika. Kutajwa kokote kwa Agora kulithibitiwa, na mtu ambaye alikuwa anaposti alionywa. Watu waliambiwa dhahiri kuwa wasiongelee kuhusu Agora na wasiposti chochote kuhusu sisi. Matukio yote kwenye kipindi hiki yangetosha kuandika kitabu cha kusisimua. Kuna wakati, ilibidi tumuhusishe mwanasheria wetu wenyewe ili kutoa onyo la dhahiri kuwa hatuwezi kuvumilia unyanyasaji wa wanachama wetu kuendelea. Sakata lote hili lilituhamasisha kuposti hiki kifuatacho:

 

What Are We Here For

 

Lakini, tulivumilia, tukaendelea kusukuma, tukaendelea kukua, na tangu mwanzoni mwa 2021, Agora ilikuwa na klabu zaidi ya 160 ndani ya nchi 70. Sasa tupo thabiti, na tupo hapa kubaki. Na huo ndio kwanza mwanzo... Moto ndio kwanza umeanza kusambaa sasa.

 

Matukio Muhimu ya Agora

Hii ni kazi inayoendelea. Bofya kwenye picha ili kuikuza. Kama unadhani tumesahau tukio la muhimu (haswa kama ni kuanzishwa kwa klabu ya kwanza ndani ya nchi, tafadhali tutumie picha za mkutano, na tutaziongeza.

 

2021

 

2021
Ago (iliyopangwa) Agora imefanikiwa kutafsiri nyenzo za msingi kwenda lugha 20. 2021 Translations
Mei 19 Klabu ya kwanza ya Agora nchini China ilianzishwa - Agora China Connectors - ikiongozwa na Aaron Leung 2021 05 China
Feb Klabu ya kwanza ya Agora nchini Kanada ilianzishwa - Stand By Me Speakers - ikiongozwa na Fred Jones na Wayne Stanton.  
Feb 14 Mfumo wa Uanachama wazinduliwa 2021 02 Membership
Jan 30 Marathoni ya Pili ya Agora iliandaliwa na Clara Manzo - masaa 36 ya mikutano ya klabu iliyofuatana 2020 01 30 Marathon
Jan 29 Majarida yenye Umakini yaliongezwa kwenye Mpango wa Kielimu 2021 01 29 Reflective Journals

 

 

2020

 

2020
Okt 21 Fred Jones alirekodi Video ya Kwanza ya mafunzo kwa ajili ya majukumu ya mkutano ya Agora. 2020 Video Tutorial
Okt 15 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Ireland ilianzishwa - Public Speakers Sligo, ikiongozwa na Kieran Timmons. 2020 10 15 Ireland
Okt 15 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Paraguay ilianzishwa - Agora Speakers Ñañe'ē, ikiongozwa na Susana Torres. 2020 10 14 Paraguay
Okt 15 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Czech ilianzishwa - Amplion Speakers, ikiongozwa na Radek Bartman. 2020 10 15 Czechia
Okt 15 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Austria ilianzishwa - Agora Speakers Vienna, ikiongozwa na Karin Silvina. 2020 10 15 Austria
Ago Klabu ya kwanza ya Agora nchini El Salvador ilianzishwa - Agora Speakers San Salvador, ikiongozwa na William Martínez.  
Ago Klabu ya kwanza ya Agora nchini Argentina ilianzishwa -  Agora Speakers Cordoba, ikiongozwa na Fabiana Alicia Fa Luchini.  
Ago 21-22 Marathoni ya Kwanza ya Agora, masaa 24 ya mikutano ya mtandaoni iliyofuatana, iliandaliwa na Clara Manzo, Ravi Bhattarai, Michael Nicholson, na Hélène Kemmere. 2020 Marathon
Ago 21 Toleo la kwanza la Mpango wa Agora wa Vijana latolewa - kilele cha juhudi ya miezi mingi kilichoongozwa na Fred Jones,  Koka Prasad,  Ravi Bhattarai 2020 Youth
Julai 25 Agora yatoa toleo jipya kabisa la wiki ambalo linajumuisha mfumo wa kujiendesha wa uundaji wa rasilimali binafsi za klabu, msaada wa lugha mbalimbali na fomu za kielekroniki za utathmini. 2020 Custom Asset
Juni 11 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Guinea-Conakry ilianzishwa - Agora Speakers Conakry, ikiongozwa na with Diané Bangaly. 2020 Conakry
Apr 1 Kwasababu ya janga linaloendelea, Agora yafanya akaunti za malipo za Zoom kuwa bure kwa klabu zote za umma ambazo zinataka kuendelea na mikutano mtandaoni. 2020 Online Meetings
Jan 20 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Ujerumani ilianzishwa- Redeclub Landshut, ikiongozwa na Monika Gräter. 2020 Germany
Jan 20 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Ukraine ilianzishwa - Agora Speakers Kharkiv, ikiongozwa na Mohammed Saif. 2020 Ukraine
Jan 13 Kitabu cha Masharti ya Mashindano kwa ajili ya mashindano yetu ya dhamira chachapishwa. 2020 Contests
     

 

2019

 

2019
Dis 19 Gea Ban Peng avunja rekodi ya mahudhurio na sherehe kubwa ya mwaka mpya kwa ajili ya Agora Speakers Singapore. 2020 Singapore
Dis 14 Nchini Ecuador, Klabu ya Kwanza ya Agora yaanzishwa - Agora Speakers Quito, ikiongozwa na Tania Soledad Guerra. klabu yavunja rekodi ya uanzilishi, ikiwa na wanachama waanzilishi 33. Nyuma yake ni klabu ya Guayaquil inayoongozwa na Hector Cedeño, ikiwa na wanachama waanzilishi 23. 2019 Ecuador
Dis 13 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Korea Kusini ilianzishwa - Seoul Agora Speakers, ikiongozwa na Sara Walsh. 2019 Korea
Dis 12 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Romania ilianzishwa - Agoramania, ikiongozwa na Gabriela Laslau. 2019 Romania
Dis 7 Klabu ya kwanza ya nchini Ukraine ilianzishwa - Agora Speakers Kharkiv, ikiongozwa na Mohammed Saif. 82106568 747581795764689 6872487241751461888 N
Dis 5 Mwongozo wa Ukufunzi wachapishwa 2019 Mentoring
Okt 23 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Philippines ilianzishwa, ikiongozwa na Celia Alamo Jacob na Fabio Aromatici. Manila
Okt 18 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Uturuki ilianzishwa, ikiongozwa na Ashney Nicolle (Ashinyi Ateghang Nicoline). Turkey
Okt 14 Kwasababu ya usaidizi wa Mitch Carson, Agora Speakers International ilizungumziwa na CNN Philippines. 2019 Cnn
Sep 30 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Ghana ilianzishwa - Agora Speakers Accra, ikiongozwa na Emmanuel Antwi 2019 Ghana
Sep 29 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Morocco ilianzishwa - Agora Speakers Rabat. 2019 Morocco
Sep 21-22 Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa ulifanyika mjini Lisbon, nchini Ureno. 71711165 2291816360917581 9069592313369460736 N
Sep 19 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Botswana ilianzishwa - Klabu ya Dirisha la Matumaini la Abigail, ikiongozwa na Moiteela Mo-Abi. 2019 Botswana
Sep 19 Jukwaa la Majadiliano Lilifunguliwa. 2019 Forums
Sep 8 "Leo tunasafiri kwenda" Shughuli ya Kielimu iliongezwa. 2019 09 08 Today We Travel To
Sep 6 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Cameroon ilianzishwa, Wazungumzaji 2035, ikiongozwa na Bw. Diangha Clifford 2019 Cameroon
Juni Klabu ya kwanza ya Agora nchini Kenya ilianzishwa - Sura ya Sani Agora Kenya  
Apr 10 Klabu ya kwanza ya Shirika ilianzishwa - kama sehemu ya (Rural Servicios Informáticos), ikiongozwa na Jose Manuel Ropero Tagua. 56902475 2375061472506527 8837797150357192704 N
Machi Klabu ya kwanza ya Agora nchini Malaysia ilianzishwa - Agora Speakers Kota Kinabalu, ikiongozwa na Johan Amilin. 71044000 10156614742666903 1349651777225490432 O
Machi Klabu ya kwanza ya Agora nchini Taiwan ilianzishwa - Wazungumzaji wa Kiingereza Wa Moto wa Taipei - ikiongozwa na Jackie Chen. 68746829 2641874659190097 2597634329865617408 O
Feb Klabu ya kwanza ya Agora nchini Mali ilianzishwa - Agora Speakers Bamako Bamako Mali

 

2018

2018
Nov 18 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Thailand ilianzishwa, ikiongozwa na Danupol Siamwalla 20190906200342
Nov 15 Mpango wa Agora wa Vijana ulitekelezwa kwa mara ya kwanza nchini Sierra Leone, ikiongozwa na Angel Zinsel. 2018 Sierra Leone
Jul 30 Agora Speakers International iliandikishwa rasmi ndani ya Umoja wa Ulaya kama Shirika. Registration
Jul 8 Mpango wa Agora wa Vijana ulizinduliwa, ukiongozwa na Fred Jones pamoja na usaidizi wa Jorge Dias, Ravi Bhattarai, na Koka Prasad. Cake
Juni Klabu ya kwanza ya Agora nchini Japan ilianzishwa, ikiongozwa na Drian Von Golden 40008533 2133134816949962 6108038326407659520 O
Machi 26 Mkutano wa kwanza wa klabu mbalimbali za kanda - Barreiro, nchini Ureno 2018 Multi Club

 

2017

 

2017
Dis Klabu ya kwanza ya Agora nchini Indonesia ilianzishwa - Jakarta Agora Speakers, ikiongozwa na Attie Ringo. 1 Jakarta2
Okt Klabu ya kwanza ya Agora nchini Ethiopia ilianzishwa - Addis Agora Speakers Club, ikiongozwa na Rajendra Singh. 37905786 1127593294062329 3993691811385180160 O
Ago Klabu ya kwanza ya Agora nchini Singapore ilianzishwa  - Agora Singapore Speakers, ikiongozwa na Gea Ban Peng. 70376698 10215279788927234 2477701572897800192 O
Ago Klabu ya kwanza ya Agora nchini Liberia ilianzishwa - Agora Speakers Monrovia Liberia
Ago Klabu ya kwanza ya Agora nchini Ureno ilianzishwa - Agora Speakers Barreiro, ikiongozwa na Jorge Dias.  21587343 1670336062979075 9135182629723282801 O
Jul Klabu ya kwanza ya Agora nchini Jordan ilianzishwa - Amman Speakers, ikiongozwa na Osama Al Mosa. 8 Oman 1
Mei Klabu ya kwanza ya Agora nchini Mexico ilianzishwa - Agora Speakers Guadalajara  
Apr Klabu ya kwanza ya Agora nchini Nigeria ilianzishwa - Agora Speakers Kaduna  
Machi 26 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Zimbabwe ilianzishwa - "Wazungumzaji wa Baadae", ikiongozwa na Patience Dube.  
Machi Klabu ya kwanza ya Agora nchini Madagascar ilianzishwa -  Agora Speakers Tana - ikiongozwa na Monique (Lene) Vieyra. 41880509 1560043187435603 8073146457449824256 O
Feb 19 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Lithuania ilianzishwa - "Agora Speakers Kaunas", ikiongozwa na Pius Abeshi. 2017 Lithuania
Feb Klabu ya kwanza ya Agora nchini Marekani ilianzishwa - Agora Central Coast Speakers  
Jan 17 Toleo la kwanza la Mwongozo wa Agora lilichapishwa. 2017 Agora Guide
Jan Klabu ya kwanza ya Agora nchini Malawi ilianzishwa - Agora Speakers Chisepo, ikiongozwa na Gosten Chikasowa 17017057 1459548100724540 8654868299724403692 O

 

 

2016

 

2016
Dis Klabu ya kwanza ya Agora nchini Uingereza ilianzishwa, ikiongozwa na Hélène Kemmere. Hellene
Nov 15 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Afrika Kusini ilianzishwa. "King's Speakers", ikiongozwa na Chris Callaghan 2016 11 South Africa
Okt Klabu ya kwanza ya Agora nchini Nepal ilianzishwa - Agora Speakers Kathmandu. Kathmandu
Okt 1 Klabu ya kwanza ya Agora nchini India ilianzishwa, na klabu ya nne duniani kote. - "Visakha Orators", ikiongozwa na Koka Prasad 2016 10 01 India
Sep 28 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Poland ilianzishwa, na klabu ya pili duniani kote - "Mówcy Gorzów", ikiongozwa na Michal Papis na Wanda Łopuszańska. 2016 09 28 Poland
Sep 23 Uandikishaji wa mafanikio wa alama ya Biashara "Agora Speakers International" Trademark1
Ago 21 Agora Speakers International ilianzishwa rasmi

 

 

 


Contributors to this page: agora and zahra.ak .
Page last modified on Monday August 30, 2021 01:43:09 CEST by agora.